Search This Blog

Friday, April 18, 2014

PICHA ZA UCHI SHILOLE MATATANI




MSANII ndani ya tasnia ya filamu na muziki, Zena Muhamed ‘Shilole’, ameuambia mtandao waDarTalk kuwa awali alipoigia kwenye tasnia ya filamu alikuwa anatafuta skendo lakini hata hivyo hakuwahi kujiweka nusu uchi ili ajulikane kwani siku ambayo atafanya hivyo ananaamini hata familia yake na hata mashabiki wanaomkubali watamuona mtu wa ajabu sana.
Msanii huyo alidai kuwa alikuwa na skendo nyingi lakini hakuwahi kuwaonesha watanzania mwili wake kama baadhi ya wasanii wanavyofanya, kwani kitendo hicho endapo angeamua kukifanya basi wazazi wake wangemchukulia kama limbukemi wa maisha ya mjini.
Kauli ya msanii huyo inakuja ili kujisafisha kwani wadau wengi wa tasnia ya filamu kwa sasa hawana hamu nayo, kutokana na vitendo vingi vinavyofanywa na wasanii wake, ambapo vingine vimekuwa vikiwahawaribu hata watoto wadogo ambao hupenda sana kutazama kazi zao.
“Awali wakati naanza filamu nilitamani sana na mimi niwe staa na nikawa natumia njia kibao lakini hakuna hata moja ambayo unaweza kusema imenichafua au kuniacha nikiwa mtupu na watu wakawa wananiona mwili wangu hakuna, lakini nashindwa kuelewa nikwanini mastaa wazima wanatumia miili yao kuongeza umaarufu wakati wanajitia doa tu,” alisema.
Hata hivyo msanii huyo aliongeza kuwa anaamini pia kwa kaisi kikubwa muziki nao umempa umaarufu sana, kwani amejizolea mashabiki wengi ndani na nje ya nchi, hasa wale wanaopenda aina ya muziki anaofanya.

STEVEN KANUMBA

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/sw/thumb/e/e7/Steven-Kanumba.jpg/220px-Steven-Kanumba.jpgSteven Charles Kanumba (8 Januari 1984, Shinyanga - 7 Aprili 2012) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchiniSteven alianza masomo yake katika shule ya msingi yaBugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.

UFUSKA KWENYE TASNIA YA FILAM TANZANIA

Moja kati ya ma director walio jipatia umaarufu baada ya kazi yake mpya kutoka itwaayo "KIBEGI" ahusishwa na metendo machafu katika kazi yake, aidha baadhi ya waigizaji hasahasa wa jinsia yakike walalamika kwa tabia iliyo ibuka kwa madirector walio wengi kwa kuwataka kimapenzi ili kupangwa katika nafasi zilizo bora kama maain character na nyinginezo.